Blogu ya EF

Picha ya juu ya kuanzia ya mandharinyuma ya ETH
Picha ya chini ya kumalizia ya mandharinyuma ya ETH
Ruka maudhui

Chapisho hili linapatikana katika 16 lugha:

Kiswahili

Kutangaza Mtandao wa Jaribio la Muungano wa Kiln

Ilichapishwa na Protocol Support Team mnamo 14 Machi 2022

Kutangaza Mtandao wa Jaribio la Muungano wa Kiln

Mtandao wa jaribio la muungano wa Kintsugi 🍵, iliyozinduliwa mwishoni mwa Desemba, umekuwa msingi muhimu wa jaribio la Muungano. Kupitia programu mbalimbali za jaribio, devnet za seva mbalimbali, shadow forks of Goerli, usambazaji wa programu na usaidizi wa jamii wa #TestingTheMerge, tumeamua maelezo ya itifaki imara na madhubuti. Kwa kuwa sasa wateja wametekeleza maelezo haya ya hivi punde, mrithi wa Kintsugi, Kiln 🔥🧱, inazinduliwa!

Kama Ethereum mainnet, safu ya utekelezaji wa Kiln ilizinduliwa kulingana na ithibati ya miamala sambamba na ithibati ya dau. Mpito kamili wa Kiln hadi ithibati ya dau unatarajiwa mapema wiki hii. Ikiwa unasoma chapisho hili baada ya tarehe 17 Machi, 2022, huenda Muungano tayari umetendeka kwenye Kiln!

Kiln inatarajiwa kuwa mtandao wa jaribio la kuungana wa mwisho kuundwa kabla ya mitandao ya jaribio la umma iliyopo kupata toleo jipya. Wasanidi programu na zana, waendeshaji wa nodi, watoa huduma za miundomsingi na wadau wanahimizwa sana kujaribu kwenye Kiln ili kuhakikisha kuna mpito bila matatizo kwenye mitandao ya sasa ya jaribio la umma.

Kintsugi, mtandao wa awali wa jaribio la kuungana, itaacha kufanya kazi wiki zijazo.

Kutumia Kiln

Kuanza

Njia rahisi zaidi ya kuanza kutumia Kiln ni kutembelea ukurasa wa mwanzo wa mtandao. Ukiwa hapo, unaweza kuongeza mtandao kwenye pochi yako ya kivinjari, kutazama wachunguzi wa tofali, kuomba fedha kutoka kwenye mfereji wa pesa, na kuunganisha kwenye mwisho wa JSON RPC. Ikiwa ungependa kuwa mthibitishaji kwenye Kiln, launchpad ya kuweka dau pia hutumia mtandao.

Wasanidi Programu na Zana

Huku Kiln ikienda hewani, sasa ni wakati wa kuhakikisha kuwa bidhaa yako inafanya kazi kama ilivyotarajiwa kupitia mpito wa ithibati wa dau na katika muktadha wa baada ya kuungana. Kama ilivyoelezwa katika chapisho la awali, The Merge itakuwa tu na athari kidogo kwenye kandarasi za seti ndogo zilizosambazwa kwenye Ethereum, ambapo hakuna inayopaswa kuwa ikivunjika. Vilevile, sehemu kubwa ya mwisho wa mtumiaji wa API inasalia imara (yaani, isipokuwa hutumii mbinu mahususi za PoW kama vile eth_getWork).

Licha ya hayo, programu nyingi kwenye Ethereum zinahusu zaidi ya miamala ya sarafu za dijitali. Kiln ni mahali ambapo unahakikisha kuwa msimbo wako kumaliza wa mbele, zana, mfumo wa michakato otomatiki na vipengele vingine nje ya mfumo hufanya kazi ilivyokusudiwa. Tunapendekeza kwamba wasanidi programu wapitie jaribio kamili na mzunguko wa usambazaji kwenye Kiln na kuripoti tatizo lolote kwenye zana au utegemezi kwenye vidumishaji vya miradi hiyo. Ikiwa huna uhakika kuhusu mahali pa kuwasilisha tatizo, tafadhali tumia hifadhi hii.

Waendeshaji Nodi

Baada ya kuungana, nodi kamili ya Ethereum itakuwa mchanganyiko wa seva ya safu ya makubaliano, inayoendesha ithibati ya dau kwenye Mnyororo Kioleza na seva ya safu ya utekelezaji, inayodhibiti hali ya mtumiaji na kuendesha hesabu zinazohusishwa na miamala. Hizi huwasiliana kupitia tundu lililoidhinishwa kwa kutumia mbinu mpya za JSON RPC, zinazoitwa Engine API.

Hivyo, waendeshaji nodi watahitaji kuendesha makubaliano na seva ya safu ya utekelezaji kwa pamoja. Yaani, ikiwa tayari unaendesha nodi kwenye Mnyororo Kioleza, sasa unahitaji pia kuendesha seva ya safu ya utekelezaji. Vivyo hivyo, ikiwa tayari unaendesha nodi kwenye mtandao wa sasa wa ithibati ya miamala, utahitaji kuendesha seva ya safu ya makubaliano.

Unaweza kupata toleo la hivi punde la seva linalotumia Kiln hapa.

Ni muhimu kusisitiza kwamba kila safu itadumisha seti huru ya marika na kufichua API zake. Hivyo API za Beacon na JSON RPC zitaendelea kufanya kazi inavyotarajiwa.

Wadau

Kama ilivyoelezwa hapo juu, wathibitishaji kwenye Mnyororo Kioleza watahitaji kuendesha seva ya safu ya utekelezaji baada ya Kuungana. Kabla ya kuungana, hili lilipendekezwa lakini iliwezekana kwa wathibitishaji kutoa vipengele hivi kwa watoa huduma wengine. Hili liliwezekana kwa sababu data tu iliyohitajika kwenye safu ya utekelezaji ni masasisho kwenye muamala wa amana.

Baada ya kuungana, wathibitishaji wanahitaji kuhakikisha kuwa miamala katika bloku wanazounda na kuthibitisha ni halali. Ili kufanya hivyo, seva ya safu ya utekelezaji inahitajika. Ingawa hili linapanua majukumu ya wathibitishaji, pia linampa mthibitishaji anayependekeza bloku haki ya ada za kipaumbele cha miamala yake inayohusishwa (ambazo kwa sasa zinaenda kwa wachimba migodi).

Ingawa zawadi za mthibitishaji zinaongezeka kwenye Mnyororo Kioleza na zitahitaji toleo jipya la baadaye ili kutolewa, ada za muamala zitaoendelea kulipwa, kuchomwa na kusambazwa kwenye safu ya utekelezaji. Hivyo, wathibitishaji wanaweza kubainisha anwani yoyote ya Ethereum kama mpokeaji wa ada za muamala.

Kiln ni mazingira bora ya wadau wa sasa ili kujifahamisha wenyewe na muktadha wa Ethereum baada ya kuungana. Tunapendekeza ujaribu kuangazia mpangilio wako wa uzalishaji kwenye mtandao na kuhakikisha kuwa unatatua tatizo lolote sasa.

Tena, the launchpad ya kuweka dau ina kiolesura rahisi cha kuanza. Fahamu kwamba kama sehemu ya ubadilishaji jina kutoka "eth2.0", ethereum/eth2.0-deposit-cli hifadhi itabadilishw ajina hivi karibuni na kuwa ethereum/staking-deposit-cli.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Kuungana ni lini?

Tarehe ya mpito ya ithibati ya dau ya mtandao mkuu wa Ethereum not haijabainishwa kutoka wakati wa chapisho hili. Chanzo chochote kinachodai vinginevyo huenda ukawa ni utapeli. Masasisho yatachapishwa kwenye blogu hii. Tafadhali chunga usalama wako!

Endapo hakuna matatizo yanayopatikana kwenye Kiln, pind tu wateja wanapohitimisha maelezo ya utekelezaji wao, mitandao ya jaribo ya Ethereum iliyopo (Goerli, Ropsten, n.k.) itapitia mabadiliko ya Muungano. Pindi tu haya yanapofanyiwa mpito na kuimarishwa, na endapo hakuna matatizo yanayopatikana, thamani ya hitilafu itawekwa kwa mpito wa mtandao mkuu. Huo tu ndio wakati itakapowezekana kukadiria tarehe kamili ya Muungano.

Kama mtumiaji wa Ethereum au mmiliki wa Ether, kuna chochote ninachohitaji kufanya?

Hapana. Ikiwa unataka kujaribu Kiln, tafadha usisite. Tunatumai kwamba wanajamii wengi watajiunga nasi katika #TestingTheMerge kwenye Kiln.

Mtandao mkuu wa Ethereum hauathiriwi na mtandao huu wa jaribio. Matangazo ya baadaye yatatolewa kwenye blogu hii kabla ya mpito wa mtandao mkuu.

Kama nodi ya mtandao, kuna chochote ninachohitaji kufanya?

Hapana. Ikiwa unaunda bloku kwenye mtandao mkuu wa Ethereum, unapaswa kufahamu kwamba baada ya Muungano, mtandao utaendeshwa kulingana na ithibati ya dau kabisa. Wakati huo, kuunda bloku hakutawezekana kwenye mtandao.

Kama mthibitishaji, ninaweza kuondoa dau langu?

Hapana. Muungano ni daraja la juu lenye utata zaidi kwenye Ethereum kufikia leo. Ili kupunguza hatari za usumbufu wa mtandao, hatua ilichukuliwa ambayo haikujumuisha badiliko lolote la mpito kutoka kwenye daraja hili la juu.

Kutoa kwenye Mnyororo Kioleza kunaweza kupatikana kuanzia daraja la juu la kwanza baada ya Muungano. Maelezo ya safu za makubaliano na utekelezaji yanaendelea.

Kwa nini Kiln?

Mtandao wa jaribio la muungano wa awali, Kintsugi, ulipewa jina baada ya sanaa ya Mjapani ya kuvunja chungu na kukikarabati kwa kutumia dhahabu na kukifanya kuwa thabiti na maridadi zaidi.

Kwa njia hiyohiyo, Kiln ni oveni ya joto la juu inayotumiwa kubadilisha udongo kuwa vifaa vigumu, kama vile vyungu au matofali 🔥🧱.

Chapisho hili limetafsiriwa kutoka Kiingereza. Kutokana na hatua hiyo, huenda lisiwe sahihi kabisa wala la sasa. Toleo halisi linaweza kupatikana katika Kiingereza.

Subscribe to Protocol Announcements

Sign up to receive email notifications for protocol-related announcements, such as network upgrades, FAQs or security issues. You can opt-out of these at any time.


Kategoria