Blogu ya EF

Picha ya juu ya kuanzia ya mandharinyuma ya ETH
Picha ya chini ya kumalizia ya mandharinyuma ya ETH
Ruka maudhui

Chapisho hili linapatikana katika 16 lugha:

Kiswahili

Tangazo la Muungano wa Mainnet

Ilichapishwa na Protocol Support Team mnamo 24 Agosti 2022

Tangazo la Muungano wa Mainnet
  • Ethereum inahamia kwenye hatua ya kuthibitisha kiwango cha sarafu ya kripto! Mpitio, unaojulikana kama Muungano, lazima kwanza uamilishwe kwenye Mnyororo Kioleza kwa toleo jipya la Bellatrix. Baada ya hatua hii, mnyororo wa uthibitishaji wa kazi utahamia uthibitishaji wa kiwango cha sarafu ya kripto baada ya kufikisha thamani mahususi ya Total Difficulty.
  • Toleo jipya la Bellatrix limeratibiwa kwa epoch 144896 kwenye Mnyororo Kioleza -- saa 11:34:47 asubuhi UTC tarehe 6 Septemba, 2022.
  • Thamani ya Terminal Total Difficulty inayochochea Muungano ni 58750000000000000000000, inatarajiwa kati ya Sept 10-20, 2022.
  • Fahamu: kama ilivyotangazwa mapema, mtandao wa jaribio wa Kiln unafungwa. Waendeshaji watafunga tarehe 6 Septemba, 2022.

Mandharinyuma

Baada ya kutia bidii kwa miaka mingi, toleo jipya la uthibitishaji wa kiasi cha sarafu ya kripto hatimaye lipo hapa! Ufanisi wa toleo jipya la mitandao yote ya majaribio ya umma sasa umekamilika na Muungano umeratibiwa wa mtandao mkuu wa Ethereum.

Muungano ni tofauti na matoleo mapya ya awali ya mtandao kwa njia mbili. Kwanza, waendeshaji wa nodi wanahitaji kusasisha safu yao ya makubaliano (CL) na safu ya utekelezaji (EL) kwa pamoja, badala ya moja tu kati ya mbili. Pili, toleo jipya linaamilisha katika awamu mbili: ya kwanza, inayoitwa Bellatrix, kwenye urefu wa epoch kwenye Mnyororo Kioleza na ya pili, inayoitwa Paris, baada ya kutimiza thamani ya Total Difficulty kwenye safu ya utekelezaji.

Taarifa ya Toleo Jipya

Wakati

Muungano ni mchakato wa hatua mbili. Hatua ya kwanza ni toleo jipya la mtandao, Bellatrix, kwenye safu ya makubaliano inayochochewa na urefu wa epoch. Hii inafuatiwa na mpito wa safu ya utekelezaji kutoka uthibitishaji wa kazi hadi uthibitishaji wa kiasi cha sarafu ya kripto, Paris, ilichochewa na kigezo mahususi cha Total Difficulty kinachoitwa Terminal Total Difficulty (TTD).

Toleo jipya la Bellatrix limeratibiwa kwa epoch 144896 kwenye Mnyororo Kioleza -- saa 11:34:47 asubuhi UTC tarehe 6 Septemba, 2022.

Paris, sehemu ya safu ya utekelezaji ya mpito, itachochewa na Terminal Total Difficulty (TTD) of 58750000000000000000000, inatarajiwa kati ya Sept 10-20, 2022. Tarehe kamili ambayo TTD inaafikiwa inategemea kiwango cha uthibitishaji wa kazi. Makadirio ya mpito yanaweza kupatikana kwenye bordel.wtf na 797.io/themerge.

Pindi tu safu ya utekelezaji inapotimiza au inapozidisha TTD, bloku inayofuata itazalishwa na mthibitishaji wa Mnyororo Kioleza. Mpito wa Muungano unasemekana kukamilika pindi tu Mnyororo Kioleza unapokamilisha bloku hii. Katika hali za mtandao za kawaida, hali hii itatendeka 2 epochs (au dakika ~13) baada ya bloku ya kwanza baada ya TTD kuzalishwa!

Lebo mpya ya bloku ya JSON-RPC, finalized, inarejesha bloku ya hivi punde iliyokamilishwa au htilafu ikiwa hakuna bloku ya baada ya muungano. Lebo hii inaweza kutumiwa na programu kuangalia ikiwa Muungano umekamilishwa. Vilevile, mikataba mahiri inaweza kuuliza opcode ya DIFFICULTY (0x44) (ilibadilishwa jina kuwa PREVRANDAO post-merge) ili kuamua ikiwa Muungano umetendeka. Tunapendekeza watoa huduma ya muundomsingi wafuatilie uthabiti wa jumla wa mtandao mbali na hali ya ukamilishaji.

Matoleo ya Mteja

Matoleo yafuatayo ya mteja yanakubali Muungano kwenye mtandao mkuu wa Ethereum. Lazima waendeshaji wa nodi watumie safu ya utekelezaji na ya makubaliano ili kusalia kwenye mtandao wakati na baada ya Muungano.

Wakati wa kuchagua programu ya kutumia, wathibitishaji wanapaswa kuwa makini haswa kuhusu hatari za kutumia programu ya wengi kwenye EL na CL. Kifafanuzi cha hatari hizi na madhara yake kinaweza kupatikana hapa. Kadirio la usambazaji wa seva teja za sasa za EL na CL na miongozo ya kubadilisha kutoka seva teja moja hadi nyingine inaweza kupatikana hapa.

Safu ya Makubaliano

JinaToleoKiungo
Lighthousev3.1.0Pakua
Lodestarv1.0.0Pakua
Nimbusv22.9.0Pakua
Prysmv3.1.0Pakua
Teku22.9.0Pakua

Safu ya Utekelezaji

JinaToleoKiungo
Besu22.7.2Pakua
Erigonv2022.09.01-alphaPakua
go-ethereum (geth)v1.10.23Pakua
Nethermindv1.14.1Pakua

Onyo: toleo la geth v1.10.22 lina suala nyeti la hifadhidata, usitumie toleo hili na ikiwa tayari umepata toleo jipya, tafadhali pata toleo jipya la v1.10.23 haraka iwezekanavyo.

Maelezo ya Toleo Jipya

Mabadiliko nyeti ya makubaliano ya Muungano yamebainishwa katika sehemu mbili:

  • Mabadiliko ya safu ya makubaliano chini ya saraka ya Bellatrix ya orodha ya maelezo ya makubaliano
  • Mabadiliko ya safu ya utekelezaji chini ya maelezo ya Paris katika hazina ya maelezo ya utekelezaji

Mbali na haya, maelezo mengine mawili yanashughulikia jinsi seva teja za safu ya makubaliano na ya utekelezaji zinavyotumika:

  • API ya Mtambo iliyobainishwa katika hazina ya api ya utekelezaji, hutumiwa kwa mawasiliano kati ya safu ya makubaliano na utekelezaji
  • Optimistic Sync, iliyobainishwa katika folda ya sync ya hazina ya maelezo ya makubaliano, hutumiwa na safu ya makubaliano kuleta bloku huku seva teja ya safu ya utekelezaji ikisawazisha na kutoa mwonekano kidogo wa kichwa cha mnyororo kutoka cha awali hadi cha sasa

Unganisha Bonasi ya Bug Bounty

Bonasi zote zinazohusiana na Muungano kwa ajli ya uhatari zimepokea kizidishaji cha mara 4 kati ya sasa na tarehe 8 Septemba. Hitilafu mbaya sasa zina thamani ya hadi $1 milioni USD.

Angalia mpango wa bonasi ya hitilafu kwa maelezo zaidi.

Maswali Yanayoulizwa Sana

Kama mwendeshaji wa nodi, ninapaswa kufanya nini?

Baada ya kuungana, nodi kamili ya Ethereum ni mchanganyiko wa seva ya safu ya makubaliano (CL), inayoendesha Mnyororo Kioleza ya uthibitishaji wa kiasi cha sarafu ya kripto na seva teja ya safu ya utekelezaji (EL), inayodhibiti hali ya mtumiaji na kuendesha hesabu zinazohusishwa na miamala. Seva teja ya EL na CL huwasiliana kupitia tundu lililoidhinishwa kwa kutumia mbinu mpya za JSON RPC, zinazoitwa Engine API. Seva teja ya EL na CL zinathibitishana kwa kutumia siri ya JWT. Waendeshaji wa nodi wanapaswa kurejelea nyaraka zao za seva teja kwa maagizo kuhusu jinsi ya kuzalisha na kusanidi thamani hii.

Yaani, ikiwa tayari ulikuwa ukitumia nodi kwenye Mnyororo Kioleza, sasa unahitaji pia kuendesha seva ya safu ya utekelezaji. Vivyo hivyo, ikiwa tayari unaendesha nodi kwenye mtandao wa sasa wa ithibati ya miamala, utahitaji kuendesha seva ya safu ya makubaliano. Ili ziweze kuwasiliana kwa usalama, lazima tokeni ya JWT ipitishwe kwa kila seva teja. Sasisho kwenye sehemu ya 'Endesha Nodi' ya tovuti ya ethereum.org ni zaidi ya hatua hizi ikiwa na maelezo zaidi.

Ni vizuri kusisitiza kuwa ingawa ni sehemu ya matoleo ya seva teja ya safu ya makubaliano, kuendesha Nodi ya Beacon ni tofauti na kuendesha Seva Teja ya Kithibitishaji. Lazima wanahisa waendeshe wote wawili, lakini waendeshaji wa nodi wanahitaji tu ya awali. Chapisho hili linaeleza tofauti kati ya vijenzi kwa maelezo ya kina zaidi.

Pia fahamu kwamba kila safu itadumisha seti huru ya marika na kufichua API zake. API za Beacon na JSON RPC zitaendelea kufanya kazi inavyotarajiwa.

Ninahitaji kufanya nini kama mwanahisa?

Kama ilivyofafanuliwa hapo juu, wathibitishaji kwenye Mnyororo Kioleza watahitaji kuendesha seva teja ya safu ya utekelezaji baada ya Muungano mbali na seva teja zao za safu ya makubaliano. Kabla ya Muungano, hili lilipendekezwa sana, lakini baadhi ya wathibitishaji wamepeleka majukumu haya kwa watoa huduma wengine wa nje. Hili liliwezekana kwa sababu data tu iliyohitajika kwenye safu ya utekelezaji ni masasisho kwenye muamala wa amana.

Baada ya kuungana, wathibitishaji wanahitaji kuhakikisha kuwa miamala ya watumiaji na bloku za mapito ya jimbo wanazounda na kuthibitisha ni halali. Ili kufanya hili, lazima kila nodi ya kioleza ioanishwe na seva teja ya safu ya utekelezaji. Fahamu kwamba wathibitishaji mbalimbali bado wanaweza kuoanishwa kwenye nodi moja ya kioleza na mchanganyiko wa seva teja za safu ya utekelezaji. Hili linapanua majukumu ya wathibitishaji lakini pia linampa mthibitishaji anayependekeza bloku haki ya ada za kipaumbele cha miamala yake inayohusishwa (ambazo kwa sasa zinaenda kwa nodi za mtandao).

Ingawa zawadi za mthibitishaji bado zinaongezeka kwenye Mnyororo Kioleza na zitahitaji toleo jipya la mtandao wa baadaye ili kutolewa, ada za muamala zitalipwa, kuchomwa na kusambazwa kwenye safu ya utekelezaji. Wathibitishaji wanaweza kubainisha anwani yoyote ya Ethereum kama mpokeaji wa ada za muamala.

Baada ya kusasisha seva teja yako ya makubaliano, hakikisha kuwa umeweka fee recipient kama sehemu ya mipangilio ya seva teja ya mthibitishaji wako ili kuhakikisha kuwa ada za muamala zimetumwa kwenye anwani unayodhibiti. Ikiwa umeweka hisa ukitumia mtoa huduma mwingine, ni jukumu la mtoa huduma wako kubainisha jinsi ada hizi zinavyogawanywa.

Staking Launchpad ina Orodha Kaguzi ya Utayari wa Muungano ambayo wanahisa wanaweza kutumia kuhakikisha kuwa wamepitia kila hatua ya mchakato. EthStaker pia wameandaa Warsha za Matayarisho ya Wathibitishaji, huku nyingine zaidi zikipangwa.

Wanahisa ambao wangependa kutumia mthibitishaji kwenye mtandao wa jaribio kwa maandalizi ya mpito wa uthibitishaji wa kiasi cha sarafu ya kripto wa mtandao mkuu wanaweza kufanya hivyo kwenye Goerli (sasa imeunganishwa na Prater), ambayo pia ina tukio la Staking Launchpad.

Kwa nini tarehe iliyokadiriwa ya Terminal Total Difficulty ni pana?

Ugumu wa nyongeza unaoongezwa kwa kila bloku unategemea kiwango cha mtandao ambacho kinabadilika. Ikiwa kiwango zaidi cha hashi kinajiunga na mtandao, TTD itatimizwa hivi karibuni. Ikiwa kiwango zaidi cha hashi kinaondoka kwenye mtandao, TTD itatimizwa baadaye. Endapo kuna upunguaji mkubwa wa viwango vya hashi, TTD Override inaweza kuratibiwa kama ilivyofanywa kwenye Ropsten.

Kama programu au msanidu wa zana, ninapaswa kufanya nini?

Kama ilivyoelezwa katika chapisho la awali, The Merge itakuwa tu na athari kidogo kwenye kandarasi za seti ndogo zilizosambazwa kwenye Ethereum, ambapo hakuna inayopaswa kuwa ikivunjika. Vilevile, sehemu kubwa ya mwisho wa mtumiaji wa API inasalia imara (isipokuwa utumie mbinu mahususi za uthibitishaji wa kazi kama vile eth_getWork).

Licha ya hayo, programu nyingi kwenye Ethereum zinahusu zaidi ya miamala ya sarafu za dijitali. Sasa ni wakati wa kuhakikisha kuwa msimbo wako kumaliza wa mbele, zana, mfumo wa michakato otomatiki na vipengele vingine nje ya mfumo hufanya kazi ilivyokusudiwa. Tunapendekeza kwamba wasanidi programu wapitie jaribio kamili na mzunguko wa usambazaji kwenye Sepolia au Goerli na kuripoti tatizo lolote kwenye zana au utegemezi kwenye vidumishaji vya miradi hiyo. Ikiwa huna uhakika wa mahali pa kuwasilisha tatizo, tafadhali tumia hifadhi hii.

Vilevile, tafadhali fahamu kwammba mitandao yote ya jaribio mbali na Sepolia na Goerli itaondolewa baada ya muungano. Ikiwa wewe ni mtumiaji wa Ropsten, Rinkeby au Kiln, unapaswa kupanga kuhamia Goerli au Sepolia. Taarifa zaidi kuhusu hii zinaweza kupatikana hapa.

Kama mtumiaji wa Ethereum au mmiliki wa Ether, kuna chochote ninachohitaji kufanya?

Iwe unatumia miamala ya sarafu za kripto za programu za Ethereum, una Ether kwenye pochi ya ubadilisanaji au ya binafsi, huhitaji kufanya chochote. Ikiwa programu, ubadilishanaji wa sarafu au pochi unayotumia ina maagizo au mapendekezo ya ziada, unapaswa kuyathibitisha kuwa yanatoka huko. Tahadhari ulaghai!

Kama nodi ya mtandao, kuna chochote ninachohitaji kufanya?

Hapana. Ikiwa unaunda bloku kwenye mtandao mkuu wa Ethereum, unapaswa kufahamu kwamba mtandao utaendeshwa kikamilifu kulingana na uthibitishaji wa kiasi cha sarafu ya kripto baada ya Muungano. Wakati huo, kuunda bloku hakutawezekana kwenye mtandao.

Je, ni nini kitakachotendeka ikiwa mimi ni muundaji bloku au mwendeshaji wa nodi na nisishiriki katika toleo jipya?

Ikiwa unatumia seva teja ya Ethereum ambayo haijasasishwa hadi toleo la hivi punde (lililoorodheshwa hapo juu), sva teja yako itasawazishwa hadi mnyororo wa bloku kabla ya mabadiliko pindi toleo jipya linapotokea.

Utakaa kweny mnyororo usiooana baada ya sheria za zamani na hutaweza kutuma Ether wala kuendesha kwenye mtandao wa Ethereum baad aya muungano.

Kama mthibitishaji, ninaweza kuondoa dau langu?

Hapana. Muungano ni daraja la juu lenye utata zaidi kwenye Ethereum kufikia leo. Ili kupunguza hatari za usumbufu wa mtandao, hatua ilichukuliwa ambayo haikujumuisha badiliko lolote la mpito kutoka kwenye toleo hili jipya.

Kutoa kwenye Mnyororo Kioleza kunaweza kuanzishwa katika toleo jipya la kwanza baada ya Muungano. Maelezo ya safu za makubaliano na utekelezaji yanaendelea.

Nina maswali zaidi, nitauliza wapi?

Jiunge na wasanidi programu wa timu ya seva teja, wanachama wa ETHStaker, watafiti na mengine mengi kwenye Simu ya Jamii ya Muungano Ijumaa, tarehe 9 Septemba saa 14:00 UTC!

Asante

Mpito wa Ethereum hadi uthibitishaji wa kiasi cha sarafu ya kripto umekuwa njiani. Asante kwa kila mtu aliyechangia kutafuta, kubainisha, kuunda, kuchanganua, kupima, kugawa, kurekebisha, au kueleza kila kitu kilichotuleta kwenye Muungano.

Kumekuwa na wachangiaji wengi sana kwa miaka mingi ambao si rahisi kuorodhesha hapa, mnajijua. Bila nyote katika eneo hili, tusingeweza kufanya mambo haya makubwa.

Kuungana ni lini? Hivi 🔜.


Asante Joseph Schweitzer na Tomo Saito kwa picha ya jalada ya chapisho hili!

Chapisho hili limetafsiriwa kutoka Kiingereza. Kutokana na hatua hiyo, huenda lisiwe sahihi kabisa wala la sasa. Toleo halisi linaweza kupatikana katika Kiingereza.

Subscribe to Protocol Announcements

Sign up to receive email notifications for protocol-related announcements, such as network upgrades, FAQs or security issues. You can opt-out of these at any time.


Kategoria