Blogu ya EF

Picha ya juu ya kuanzia ya mandharinyuma ya ETH
Picha ya chini ya kumalizia ya mandharinyuma ya ETH
Ruka maudhui

Chapisho hili linapatikana katika 16 lugha:

Kiswahili

Kutafsiri blogu ya Msingi wa Ethereum

Ilichapishwa na Ethereum.org Team mnamo 31 Agosti 2022

Kutafsiri blogu ya Msingi wa Ethereum

Tangu chapisho la kwanza Desemba 2013, blogu ya Msingi wa Ethereum (EF) imekuwa njia ya msingi ya mawasiliano kwa timu ndani ya EF. Kutoka kwenye matangazo kuhusu matukio, to mawimbi ya ruzuku, maboresho ya itifaki, taarifa za mara kwa mara kutoka kwenye timu mahususi au kujadili maono na ratiba ya Ethereum, blogu imekuwa rasilimali muhimu kwa wale wanaotaka kuendelea kufahamu kinachojiri.

Hata hivyo, kumekuwepo na tatizo kubwa: licha ya jamii yetu ya Ethereum ya kimataifa, taarifa hii imekuwa ikipatikana tu kwa Kiingereza. Kufikia taarifa hizi ni changamoto kwa mabilioni ya watu wasiozungumza Kiingereza kote duniani.

ethereum.org na Mpango wa Tafsiri

Tayari tumeona ethereum.org ikionyesha njia inayoendeshwa na jamii yenye ufanisi kwa tafsiri za Ethereum. Mwaka wa 2019, ethereum.org ilianza kutafsiri maudhui yake ya programu huria ya elimu katika lugha mbalimbali. Kwa muda mrefu, jitihada hii imepanda hadi lugha 48 na mamilioni ya maneno yaliyotafsiriwa kila mwaka na maelfu ya wachangiaji wa kujitolea.

Ushirikishaji wa jamii

Kipengele muhimu cha ufanisi wa Mpango wa Tafsiri ni maelfu ya wachangiaji wake wenye shauku. Kwa wengi, kutafsiri ni moja ya njia muhimu wanazoweza kuchangia kwenye ikolojia ya Ethereum ili kujifunza, kufunza na kuishukuru jamii.

Ethereum.org kwa sasa ina:

  • Watafsiri 3,800 wanaochangia
  • Lugha 48 moja kwa moja kwenye tovuti
  • Maneno milioni 2.9 yalitafsiriwa 2021
  • Maneno milioni 1.9 yalitafsiriwa 2022 kufikia sasa

Je, watu wanatumia tafsiri?

Jaribio la timu ya ethereum.org kuhusu tafsiri linaonyesha thamani ya kufanya maudhui ya Ethereum kupatikana katika lugha mbalimbali. Hoja kuu imewekwa bayana: kadri tunavyotafsiri maudhui zaidi, ndivyo asilimia kubwa ya ya watumiaji kwa jumla wanaenda kwenye kurasa zilizotafsiriwa. Mtindo umekuwa imara huku maudhui yaliyotafsiriwa yakiongoza asilimia 5 ya kurasa zilizotazamwa baadaye 2019 hadi asilimia 22 kufikia sasa ya jumla ya kurasa zilizotazamwa. Hii inaonyeshwa hali ya uelewa — hata wanajamii walio na ustadi wa wa Kiingereza huripoti wakipendelea kusoma kwa lugha yao ya asili.

Tafsiri kamilifu zaidi ya maudhui ya ethereum.org iko katika Kichina Kilichorahisishwa. Matokeo? Asilimia 8 ya watumiaji wote wa ethereum.org ni kwenye toleo la Kichina Kilichorahisishwa cha tovuti.

Tafsiri kila kitu!

Wakati ufanisi wa tafsiri kwenye ethereum.org ulipodhihirika, nafasi nyingine za wazi za tafsiri ziliibuka.

Ethereum Staking Launchpad, mwongozo shirikishi wa kuwa mwanahisa pekee na kuweka mthibitishaji, umetafsiriwa katika lugha 20.

Tangu mapema 2022, pia tumeongeza baadhi ya tafsiri ili uteue machapisho ya blogu (mfano maboresho ya mtandao wa jaribio ya hivi majuzi). Hata hivyo, hili lilikuwa suluhisho la muda mfupi ikizingatiwa kwamba blogu haikuunga mkono kufanya huduma kuwa ya kimataifa. Tafsiri hazikuorodheshwa, kutafutwa kwa urahisi wala kutabiri unachotafuta.

Taarifa za blogu: ni nini kilichobadilika?

Hapa chini pana maelezo mafupi kuhusu kazi ambayo tumefanya kufikia sasa na tunachopanga kuboresha baadaye.

Usaidizi wa kufanya huduma ya kimataifa

Kuanzia uzinduzi wa leo, blogu ya EF ina usaidizi kamili wa kufanya huduma ya mataifa, kumaanisha unapochagua lugha ili uone blogu (mfano, blog.ethereum.org/zh/), utaweza kuona machapisho katika lugha yako lengwa. Pia hii inaboresha safu za lugha za kulia hadi kushoto, kama Kiarabu.

Maboresho ya utendaji

Kama sehemu ya kujenga blogu upya, tulihamisha msimbo hadi muundomsingi wa teknolojia mpya kabisa (kutoka Jekyll hadi Next.js). Next.js ni mfumo wa wavuti wa kisasa ulioboreshwa kwa utendaji wa mtumiaji. Tunatarajia maboresho ya utendaji ili kutambuliwa na kila mtu, lakini wale wasio na uwezo wa kufikia intaneti ya kasi ya juu wanapaswa kuona maboresho makubwa zaidi katika kasi za kupakia na hali ya mtumiaji.

Maboresho ya ufikiaji

Uboreshaji pia unaimarisha ufikiaji wa blogu. Kama mfumo wa mtindo ulipo tunaotumia huzingatia kwa karibu Miongozo ya Ufikiaji wa Maudhui ya Wavuti (WCAG), kuna uboreshaji mkubwa katika ufikiaji haswa kwa watumiaji wa wasomaji wa skrini.

Mipango ya baadaye

Ingawa blogu hii mpya ni uboreshaji wa juu kutoka kwenye toleo la awali, bado tuna matoleo zaidi ambayo tungependa kufanya.

Usajili wa barua pepe

Kama sehemu ya uboreshaji wa blogu, tumeimarisha usaidizi kwa wasomaji wa RSS. Kwa hivyo badala ya kuhitajika kuangalia blogu mara kwa mara kwenye mlisho wako wa Twitter kwa taarifa, unaweza kujisajili kwenye mlisho wa RSS.

Hata hivyo, mwaka wa 2022, watu wanatarajia chaguo ambalo ni bayana zaidi: arifa za barua pepe. Hiki ndicho kinachofuata kwenye orodha yetu ya vipaumbele, kwani tunaamini kwamba haya yatakuwa maboresho makubwa katika hali ya mtumiaji blogu kwa wote.

Lugha zilizoongezwa

ethereum.org imeonyesha uhitaji wa lugha mbalimbali. Leo tunazindua pamoja na matumizi ya lugha 16 lakini tunatarajia kuongeza machaguo haya hivi karibuni. Hili linatufikisha kwenye hoja inayofuata...

Jihusishe!

Je, ungependa kusaidia kutafsiri blogu ya EF?

Pata kila kitu unachohitaji ili uhusishwe na mpango wetu wa tafsiri.

Asante kwa kutusaidia kuboresha upatikanaji wa taarifa kwa mamilioni ya wasomaji kote ulimwenguni!

Chapisho hili limetafsiriwa kutoka Kiingereza. Kutokana na hatua hiyo, huenda lisiwe sahihi kabisa wala la sasa. Toleo halisi linaweza kupatikana katika Kiingereza.

Kategoria