Blogu ya EF

Picha ya juu ya kuanzia ya mandharinyuma ya ETH
Picha ya chini ya kumalizia ya mandharinyuma ya ETH
Ruka maudhui

31 Agosti 2022

ETH.org

Kutafsiri blogu ya Msingi wa Ethereum
Kutafsiri blogu ya Msingi wa Ethereum

na Ethereum.org Team

Tangu chapisho la kwanza Desemba 2013, blogu ya Msingi wa Ethereum (EF) imekuwa njia ya msingi ya mawasiliano kwa timu ndani ya EF. Kutoka kwenye matangazo kuhusu matukio, to mawimbi ya ruzuku, maboresho ya itifaki, taarifa za mara kwa mara kutoka kwenye timu mahususi au kujadili maono na ratiba ya Ethereum, blogu imekuwa rasilimali muhimu kwa wale wanaotaka kuendelea kufahamu kinachojiri. Hata hivyo, kumekuwepo na tatizo kubwa: licha ya jamii yetu ya Ethereum ya kimataifa, taarifa hii imekuwa ikipatikana tu kwa Kiingereza. Kufikia taarifa hizi ni changamoto kwa mabilioni ya watu wasiozungumza Kiingereza kote duniani.

na Protocol Support Team

Ethereum inahamia kwenye hatua ya kuthibitisha kiwango cha sarafu ya kripto! Mpitio, unaojulikana kama Muungano, lazima kwanza uamilishwe kwenye Mnyororo Kioleza kwa toleo jipya la Bellatrix. Baada ya hatua hii, mnyororo wa uthibitishaji wa kazi utahamia uthibitishaji wa kiwango cha sarafu ya kripto baada ya kufikisha thamani mahususi ya Total Difficulty. Toleo jipya la Bellatrix limeratibiwa kwa epoch 144896 kwenye Mnyororo Kioleza -- saa 11:34:47 asubuhi UTC tarehe 6 Septemba, 2022. Thamani ya Terminal Total Difficulty inayochochea Muungano ni 58750000000000000000000, inatarajiwa kati ya Sept 10-20, 2022. Fahamu: kama ilivyotangazwa mapema, mtandao wa jaribio wa Kiln unafungwa. Waendeshaji watafunga tarehe 6 Septemba, 2022.

14 Machi 2022

Protocol

Kutangaza Mtandao wa Jaribio la Muungano wa Kiln

na Protocol Support Team

Mtandao wa jaribio la muungano wa Kintsugi 🍵, iliyozinduliwa mwishoni mwa Desemba, umekuwa msingi muhimu wa jaribio la Muungano. Kupitia programu mbalimbali za jaribio, devnet za seva mbalimbali, shadow forks of Goerli, usambazaji wa programu na usaidizi wa jamii wa #TestingTheMerge, tumeamua maelezo ya itifaki imara na madhubuti. Kwa kuwa sasa wateja wametekeleza maelezo haya ya hivi punde, mrithi wa Kintsugi, Kiln 🔥🧱, inazinduliwa! Kama Ethereum mainnet, safu ya utekelezaji wa Kiln ilizinduliwa kulingana na ithibati ya miamala sambamba na ithibati ya dau. Mpito kamili wa Kiln hadi ithibati ya dau unatarajiwa mapema wiki hii. Ikiwa unasoma chapisho hili baada ya tarehe 17 Machi, 2022, huenda Muungano tayari umetendeka kwenye Kiln! Kiln inatarajiwa kuwa mtandao wa jaribio la kuungana wa mwisho kuundwa kabla ya mitandao ya jaribio

Kategoria